jaridahuru

Mitandao

VYUONI: WANAFUNZI 100 WAKOSA PA KULALA BAADA YA BWENI LAO KUUNGUA, WADAI CHANZO NI MFUMO WA UMEME



Kilosa. Wanafunzi 100 wa Shule ya Sekondari ya Kilimo ya Kilosa, hawana mahali pa kulala baada ya bweni lao kuteketea kwa moto jana asubuhi.

Mkuu wa shule hiyo, Erasto Luandara alisema moto huo uliotokea wakati wanafunzi hao wakijiandaa kuingia madarasani hakijafahamika.

“Mfumo wa umeme katika shule hii umechakaa na mara ya mwisho ulifanyiwa ukarabati mwaka 2003 na Danida,” alisema mkuu huyo wa shule.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo alitembelea shuleni hapo baada ya tukio hilo na kuwapa pole wanafunzi na uongozi wa shule kwa tukio hilo.

Tarimo alisema tayari Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imechukua hatua za kusaidia upatikanaji wa magodoro na madaftari kwa ajili ya wanafunzi waliokumbwa na mkasa huo.

Mkuu huyo wa wilaya pia alisema amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri kuandaa ripoti kuhusu hali ya shule hiyo iliyojengwa katika miaka ya 80 kwa msaada wa Serikali ya Cuba, ili ripoti hiyo iwasilishwe katika ngazi za juu na kufanyiwa kazi.

Related

Vyuoni 3846259065635074167

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item