KIMATAIFA: Zoezi la uchaguzi mkuu Afrika Kusini. Zuma apewa nafasi kubwa.
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/kimataifa-zoezi-la-uchaguzi-mkuu-afrika.html
Uchaguzi mkuu unaendelea Afrika Kusini ili kuichagua serikali ya nne baada ya nchi hiyo kujikwamua kutoka katika mikono ya makuburu.
Chama cha African Nationa Congress (ANC) kinapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kitendo ambacho kitamrudisha Rais Jacob Zuma ikulu ili kukamilisha awamo yake ya pili.
Ikumbukwe kuwa huu ndio uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika katika nchi hiyo baada ya kumpoteza shujaa na Rais wa kwanza wa kiafrica wa taifa hilo. Vyanzo Mbali mbali kupitia shirika la BBC vilieleza kuwa uchaguzi unaendelea kwa amani na utulivu wa hali ya juu.
Hata hivyo, chama cha ANC kinapewa nafasi kubwa ya kushinda kwa asilimia 60% ya kura zote ingawaje katika kura za maoni umma ulionesha kutoridhishwa na utendaji wa serikali iliyokuwa madarakani.
Wananchi wa taifa hilo waliozaliwa baada ya Apatheid mwaka 1994, wanapiga kura kwa mara yao ya kwanza ingawa takwimu zinaonesha kuwa ni theluthi moja tu ya wananchi hao waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura. Lehlohonolo Mafausu mwenye umri wa miaka 18 aliambia BBC kuwa alifurahi sana kuweza kupiga kura kwa mara yake ya kwanza.
"Watu wengi walipoteza maisha yao kunipa nafasi hii ya uhuru wa kumchagua rais nimpendae" Alisema Binti huyo.
Wanachi wakiwa tayari kupiga kura na shahada zao |
Ulinzi umeimarishwa katika miji yote yenye upinzani wa kisiasa ili kulinda amani.
Wapinzani wakuu wa ANC wanategemewa kuwa Democratic Alliance (DA) chama kinachoongozwa na mpiganaji dhidi ya Apatheid Helen Zille ambae pia anajaribu kuliona lango la ikulu.
Hata hivyo chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) kilicho anzishwa mwaka jana na aliyekuwa kiongozi wa Vijana wa ANC Julius Malema kinatarajia kupata nafasi ya viti vya ubunge kwa mara ya kwanza.
Tutaendelea kuwajulisha Kadri Taarifa zitakavyo tufikia.