jaridahuru

Mitandao

KIMATAIFA: SUDANI KUSINI WAKIUKA SAINI YA MAKUBALIANO YA AMANI WAINGIA VITANI TENA


Saa chache tu baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa usitishaji mapigano nchini Sudan kusini Malumbano yameibuka .

Sasa Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wanalaumiana kila upande ukimshutumu mwenzake kuvunja makubaliano hayo yaliyosainiwa ijumaa.

Hata hivyo kiongozi wa waasi Riek Machar anasema bado ameazimia kutekeleza makubaliano hayo licha ya kwamba anasema serikali ya rais Salva Kiir inavunja mapatano hayo.

Machar amesema kuwa majeshi ya UPDF ya Uganda ambayo yamekuwa yakivamia maeneo inayoyadhibiti haijaafiki mkataba uliotiwa sahihi huko Adiss Ababa kati yake na Rais Salva Kiir.
Aidha msemaji wa jeshi la serikali, Kanali Philip Aguer, amesema waasi hao wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa Bentiu .

Upinzani umepinga madai hayo.
Machar amesema kuwa angetaka mazungumzo zaidi na serikali kuhusu hilo, lakini amesema anafahamu kuwa Rais hana uwezo wa kudhibiti majeshi yote yanayopigana kwa upande mmoja na majeshi ya serikali kama vile majeshi ya Uganda na wapiganaji kutoka Darfur.
Serikali ya Sudan Kusini pia imelaumu upande wa waasi kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano saa chache tuu baada ya mkataba huo kutiwa saini.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Ijumaa, na yalikusudiwa kumaliza vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni moja kuhama makwao.

Chanzo: BBC

Related

Kimataifa 1946858872793829680

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item