CBE DOM: Wanaojiuza waanikwa Instagram
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/cbe-dom-wanaojiuza-waanikwa-instagram.html
Mitandao ya kijamii ni njia moja wapo ya kupata habari na ku 'socialize' na jamii inayotuzunguka lakini kwa wengine imekuwa sivyo kabisa. Baadhi ya watu wanaitumia vibaya mitandao hiyo kuwachafua wenzao kwa sababu wanazo zijua wao. katika tukio la hivi karibuni, mtu anaedhaniwa kuwa ni mmoja wa wanafunzi wa chuo cha CBE kampasi ya Dodoma amewachafua wanafunzi wenzake kwa kuweka picha zao na kuandika maneno ya kejeli juu yao akidai wanajiuza.
Katika mahojiano na baadhi ya wanafunzi walionesha kukerwa na jambo hilo, walidai kuwa ni majungu tu na chuo hicho kikongwe nchini, maana hakuna anayejiuza katika chuo hiko na kudai kuwa ni chuo chenye maadili isipokuwa watu wasio kuwa na kazi maalum na wanaotaka sifa kupitia chuo hiko ndio wanaozusha habari hizo.
Katika picha zaidi instagram, jamaa huyo anaepost hizo habari anatumia akaunti feki ya 'lee_in_boy' anazidi kupost habari chafu kuhusu wanafunzi hao na kudai kuwa baadhi yao ni mashoga na wamefumaniwa.
Vyanzo zaidi vilisema kuwa habari hizo zimeripotiwa na uchunguzi unaendelea kubaini ni nani anae fanya mchezo huo mchafu