jaridahuru

Mitandao

BUNGENI : UKAWA WAPIGWA "STOP" BUNGENI




SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema ni marufuku kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya shughuli zake ndani ya Bunge la Bajeti.

Alisema hayo juzi bungeni baada ya
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kutangaza baraza
kivuli la mawaziri na kusema hicho ndiko kikosi cha ukawa ndani ya
Bunge.


Spika Makinda alimtaka Mbowe kuhakikisha
Ukawa inafanya kazi zake nje ya Bunge na si ndani ya Bunge kwani
wanapokuwa ndani ya Bunge wanakuwa ni kambi ya upinzani bungeni na si
vinginevyo.
“Ukawa ndani ya Bunge haipo,
mnakumbuka shuka kumekucha, baraza lenu ni International Standard na
miaka ya nyuma nilishawahi kuwashauri kitu kama hicho lakini mkakidharau
na kuona hakina maana, nawapongeza sana, lakini mmekumbuka shuka
kumekucha,”
aliongea Makinda


Pia Spika Makinda alilitaka baraza hilo kivuli kutoa ushirikiano na wabunge wengine ili kufanya kazi ya kuendeleza watu.


“Watanzania
hawajui nani anatoka wapi ila wanachotaka ni maendeleo yatakayosaidia
kuboresha hali zao za maisha, wanataka kuona barabara nzuri na hata
mazao yao yananunuliwa,”
aliongeza

Uteuzi huo ulihusisha vyama vya Chadema,
CUF na NCCR Mageuzi ambapo baraza hilo kivuli lina mawaziri 29 ambapo
watashika nafasi za uongozi katika kipindi kilichobaki kuelekea uchaguzi
mkuu mwakani.

Related

Habari Mpya 7684164797907990668

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item