AFYA: Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani Kitaifa yaadhimishwa Mbeya.
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/afya-siku-ya-msalaba-mwekundu-duniani.html
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaendelea kupanua wigo wa ushirikiano na Sekta Binafsi katika utoaji wa Huduma za Afya nchini ili kuboresha huduma hizo kwa wananchi.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dokta Seif Rashid, amesema hatua hiyo ndiyo njia pekee ya kusaidia ufikishaji wa huduma za afya kwa kila Mtanzania kwa sababu bado sekta binafsi zina nafasi kubwa ya kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Ni kwenye Kilele cha Sherehe za Chama Cha Msalaba Mwekundu nchini, ambazo Kitaifa zimefanyika mkoani Mbeya, Waziri wa Fedha, Dokta Seif Rashid, amebainisha mpango huo wa Serikali katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani hapa, Deudatus Kinawiro.
Waziri Rashid, pia amesema kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya chama cha Msalaba Mwekundu kuhusu matumizi ya nembo ya chama hicho, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaangalia uwezekano wa kubadili nembo zinazotumika kwenye magari yake ya wagonjwa ili kuzitofautisha nembo hiyo.
Awali, Makamu Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini, Dokta Zainab Gama, ameitaka Serikali kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na matumizi yasiyo sahihi ya nembo hiyo.
Chama cha Msalaba Mwekundu Duniani kimeanzishwa mwaka 1863 ambapo hapa Tanzania kimeanzishwa mwaka 1962 kwa Sheria namba 71 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.