HISTORIA YA MWANAHARAKATI STEVE BIKO
http://jaridahuru.blogspot.com/2016/06/historia-ya-mwanaharakati-steve-biko.html
Tukizungumzia mwanaharakati wa haki za watu weusi wengi wanajua
bishop desmond tutu, Nelson Mandela, Winnie Mandela na wengine wengi
ambao walishiriki katika harakati za ukombozi wa watu weusi nchini
afrika kusini.
Leo nataka umjue mwanaharakati aliechangia kwa kiasi kikubwa katika
kuanzisha harakati za kupigania haki za watu weusi nae si mwingine bali
ni Steve Bantu Biko.
Steve Biko alikuwa akifahamika kama mwanaharakati anayepiga vita
dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, mnamo miaka ya 1960 na
1970.
Biko alikuwa kiongozi wa wanafunzi, baadae akaanzisha vuguvugu la Black Consciouness Movement.
Vuguvugu hili lilipata nguvu sana na kuenea karibuni katika miji mingi yenye idadi kubwa ya watu weusi.
Mauti yalimfikia baada ya kutiwa mbaroni na kuteswa na maaskari wa
serikali ya kibaguzi. Biko alijulikana kama jabali la harakati dhidi ya
ubaguzi wa rangi.
Wakati yupo hai, alikuwa akiandika sana masuala ya harakati za
kujaribu kuwatia nguvu watu weusi na aliweza kuwa maarufu kwa wito wake
wa kusema kwamba “black is beautiful” akimaanisha kwamba “mtu mweusi ni
mzuri.”
Alielezea maana ya msemo huu ni: “mtu, ni sawa kama ulivyo mtu, lakini anza kujiangalia mwenye ukiwa kama binaadamu.
Stephen Bantu Biko alizaliwa mjini King Williams Town, ndani ya jimbo
la Eastern Cape nchini Afrika Kusini. Biko alikuwa mwananfunzi wa Chuo
Kikuu cha Natal Medical School.
Hapo awali Biko alikuwa akijishughulisha na masuala ya kutafuta “Umoja wa Umma wa Wanafunzi Afrika Kusini”.
baada ya kuweza kuwaadikisha watu weusi, wahindi, na watu weupe pia,
kwamba wakiwa kama wanafunzi wanahitaji jumuiya itakayokuwa inawaangalia
wanafunzi.
Kwa mpango huo aliweza kufanikisha kuanzishwa kwa Jumuiya ya
Wanafunzi nchini Afrika ya Kusini, kwa Kiingereza: South African
Students’ Organisation mnamo miaka ya 1968, na Biko akachaguliwa kuwa
kama rais wa kwanza wa juimuiya hiyo.
SASO pia ilikuwa na mahusiano ya kisiri na jumuiya ya Harakati za
kujitambua kwa watu weusi. Mke wa Biko Ntsiki Mashalaba, alikuwa
mchangiaji mzuri wa kundeleza jumuiya ya “Harakati za kujitambua kwa
watu weusi”.
Mnamo mwaka 1972 Biko akawa rais wa kuzuga kuwa ndio rais anaeangalia kanuni za watu weusi .
Biko aliwekewa vikwazo wakati wa kipindi cha ubaguzi wa rangi
umeshamiri mnamo Machi mwaka 1973. Lengo kuu la kumvisha kiremba cha
ukoka bwana Biko, walimaansha ya kwamba Biko haruhusiwi kuzungumza na
zaidi ya mtu mmjoa kwa wakati mmoja.
Biko aliwekewa hadi mipaka katika baadhi ya sehemu asikanyage kabisa yaani.
Pia hakuruhusiwa kuzungumza mbele ya hadhara. Vile vile ilikatazwa
kabisaa kuzungumzia dondoo za Biko alizokuwa akisema, ikiwemo tamko au
maneno yoyote yale azumngumzayo bwana Biko.
Wakati Biko wamemuwekea vikwazo, harakati zake za kinchi zilizuiliwa katika jimbo la Eastern Cape, mahali alipozaliwa Biko.
Baada ya Biko kurudi kule kwao alikozaliwa, akaanzisha tena jamii
fulani iliyokuwa inaitwa “Jamii shinani” iliyoegemea hasa katika kutaka
watu kujitegemea wenyewe , jumuiya ilibeba taasis mbambali ikiwemo,
community clinic, Zanempilo, the Zimele Trust Fund (ambaye baadae ilitoa
msaada kwa familia yake wakati Biko alivyofungwa kisiasa), Njwaxa
Leather-Works Project na Ginsberg Education Fund.