jaridahuru

Mitandao

ELIMU: 58,037 WALIOOMBA MIKOPO BODI 2014, WALIOPATA KUTANGAZWA. MALIPO YA MAFUNZO KWA VITENDO KULIPWA WIKI IJAYO



BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HELSB), imesema kuwa itatangaza rasmi majina ya wanafunzi waliokidhi vigezo vya kupata mkopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
 
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu na Mawasiliano, Cosmas Mwaisombwa, kwamba mchakato wa upokeaji maombi kupitia mtandao ulikamilika Julai 31.

“Tumepokea maombi 58,037 na mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo utakamilika baada ya majina ya wanafunzi waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) yatakapowasilishwa rasmi kwenye bodi, kwani tunategemea taarifa muhimu kutoka kwenye tume hiyo ili kuepuka udanganyifu,’’alisema.

Mwaisombwa alisema kuwa pia serikali inatoa mikopo kwa wanafunzi wa nje waliopata udhamini wa kusoma nchi rafiki na Tanzania ili kuwawezesha kujikimu.

Aliongeza kuwa malipo ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambao hawajapata, yatakamilika kufikia wiki ijayo.

Related

Habari Mpya 219349895039442127

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item