WORLD CUP: UFAHAMU 'BRAZUCA' MPIRA UTAKAO TUMIKA KATIKA KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL (KISWAHILI)
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/world-cup-ufahamu-brazuca-mpira-utakao.html
Unaikumbuka Jabulani? kumbe mfuatiliaji mzuri au sio? zikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa kombe la dunia 2014, leo Jarida Huru inakuletea Adidas Brazuca ambao ndio Mpira rasmi wa Kombe la dunia 2014 kule Brazil. Mpira huu unatengenezwa na kampuni ya adidas ambayo ni mshirika katika wa FIFA na msambazaji wa mipira ya kuchezea Kombe la dunia kuanzia mwaka 1970. Huu ndio mpira wa kwanza rasmi kupewa jina na mashabiki na wapenzi wa soka.
Jina la Brazuca lina maanisha maisha halisi ya kibrazili hasa pale wananchi wa daraja la tatu walipokuwa wanahamia kwenda nchi zingine kutokana na kudhorora kwa uchumi katika nchi yao kulikotokana na uongozi wa kikatili wa kijeshi.
Jina hili lilitajwa rasmi Jumapili Septemba 2012. Lilichaguliwa kwa kura za mashabiki amabazo zilizo andaliwa na Uongozi wa ngazi ya mtaa wa Adidas, uchaguzi ulioshirikisha takribani mashabiki milioni moja.
Jina Brazuca lilichaguliwa kwa asilimia 77.8% ya kura zote mbele ya majina mengine mawili Bossa Nova (14.6% ya kura) na Carnavalesca (7.6% ya kura zilizo pigwa).
UUNDWAJI
Mpira huu ni muendelezo wa Adidas Tamgo 12 ikiwa na mipira na ngozi sawa ila muundo tofauti.
Fasihi ya mauzo ya Adidas inadai kuwa;
- Mpira wa Brazuca una vipande sita maalum ambavyo vimeunganishwa pamoja kuuweka mpira katika uzito sawa muda wote hata katika hali ya mvua.
- Kuna jopo za tofauti kabisa zinazoleta mapinduzi katika mchezo kwa kuwa na kasi na kuhimili kasi na umbo duara.
- Mpira wa ndani wa Brazuca imeundwa na mpira maalum na kuwa na duta inayohitajika.
- Mpira huo una unyororo wa kufanana na Adidas Finale 13 ambao ni mpira rasmi kwa ajili ya Klabu Bingwa ulaya inayozidi ya Jabulani mpira uliochezewa kombe la dunia afrika kusini miaka minne iliyopita.
- Mpira wa brazuca ni mweupe, wenye uduara na rangi zenye kuitambulisha nchi ya Brazili.
UTAMBULISHO
Adidas iliutambulisha mpira wa Brazuca katika tukio la kuutambulisha mpira huo tarehe 3 desemba 2013 utambulisho uliofanyika Rio de Janeiro, Parque Lage
Mpira huu umepitia majaribia mbali mbali hadi kuchaguliwa kuwa katika viwango vya FIFA.